Home Uncategorized AZAM FC YAPANIA KUFANYA MAKUBWA MBELE YA WAZIMBABWE

AZAM FC YAPANIA KUFANYA MAKUBWA MBELE YA WAZIMBABWE


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa upo tayari kupeperusha bendera ya Taifa Kimataifa kwa kupata matokeo chanya mbele ya Triangle FC ya Zimbabwe.

Mchezo huo ambao unatarajiwa kuchezwa kati ya Septemba 13-15 uwanja wa Chamazi ni wa hatua ya kwanza ya Kombe la Shirikisho utapingwa majira ya saa 10:00 jioni.

Idd Cheche, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa maandalizi yanakwenda sawa na kikosi kipo vizuri kupeperusha bendera ya Taifa.

“Tunatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu na kila mchezaji anahitaji kupata matokeo ni suala la muda na mashabiki watupe sapoti kwa kuwa tunaanza nyumbani kisha tunakwenda kumaliza tukiwa ugenini,” amesema. 

SOMA NA HII  KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA AZAM FC HIKI HAPA, NI MOTO BALAA