Home Uncategorized HAWA NDIO WAPINZANI WA YANGA KIMATAIFA

HAWA NDIO WAPINZANI WA YANGA KIMATAIFA

TOWNSHIP Rollers ni wapinzani wa Yanga kimataifa kwenye mchezo wa awali wa Ligi ya mabingwa unaotarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 9-11 nchini Botswana na ule wa marudio kati ya Agosti 23-25.

Township ni mabingwa mara nne mfululizo wa Ligi ya Botswana tangu 2015/16 hadi 2018/19 itamenyana na Yanga ambayo haijafanikiwa kutwaa taji mara mbili mfululizo na mara ya mwisho kutwaa taji la ligi ilikuwa ni msimu wa mwaka 2016/17 nyuma yake ilitwaa taji hilo mara mbili mfululizo.

Itakuwa si mara ya kwanza kwa Yanga kumenyana na Township Rollers kwenye michuano hii ambapo mwaka 2018 zilimenyana katika mchezo wa hatua ya kwanza uliochezwa Dar es Salaam uwanja wa Taifa, Yanga ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 na ziliporudiana nchini Botswana matokeo yalikuwa suluhu ya bila kufungana 

Yanga iliondolewa kwa kufungwa jumla ya mabao 2-1, kama Yanga itavuka hatua hii itaenda kupambana na mshindi wa mechi kati ya Green Mamba ya Eswatini na Zesco ya Zambia.

SOMA NA HII  JEMBE JIPYA SIMBA KUTUA KESHO, NDANI YA SPOTIXTRA JUMAPILI