Home Burudani KUMBE CHIDI BEENZ ALIKUWA MTU WA MIZINGA, ALIMUIBUKIA MPAKA WAZIRI WAKE

KUMBE CHIDI BEENZ ALIKUWA MTU WA MIZINGA, ALIMUIBUKIA MPAKA WAZIRI WAKE


 MSANII wa muziki wa Hip Hop, mkongwe Chidi Beenz amesema kuwa zama zile alipokuwa kwenye matumizi ya madawa ya kulevya jambo moja alilokuwa analijua ilikuwa ni kupiga mizinga wale wote ambao alikuwa na namba zao za simu.

Nyota huyo ambaye utunzi wake wa kipekee pamoja na sauti yake kali bado inabamba kwa mashabiki na dunia kiujumla kila anapopata nafasi ya kuonyesha kipaji chake ambacho kinampa mkate wake wa kila siku.

Ngoma ya Dar Stand Up ilibamba miaka ya 2011 na bado ikipigwa inachezeka iliweza kumpa tuzo ya Mwanzamuziki bora wa Hip Hop kwenye tuzo za Kili Music Award.

Chid ameweka wazi kwamba bado anaamini ana kipaji na uwezo wake upo ila zama za matumizi ya madawa ya kulevya alipoteza kumbukumbu zaidi ya kuishia kuwapiga miziga washkaji zake.

“Nilikuwa nimepoteza kumbukumbu, haikuwa rahisi kumkumbuka nani ni nani ila ninachokumbuka kwa wale ambao walikuwa na namba zangu za simu ama nimepta tu  namba zao basi ilikuwa nikikupigia lazima nikuombe nyekundu moja ama namna gani ila hela kwanza.

“Nakumbuka niliwahi kumpigia simu yule ambaye alikuwa Waziri wa Wizara yetu ya Sanaa,(Nnape Nnauye) bila kujua nikaanza kupiga naye stori sasa nikashtuka, akaanza kuniambia Chid, nakuskia, ongea, basi nikamchunia na kumuambia nilikuwa nakupa salamu,” .

SOMA NA HII  KASINO YA MTANDAONI, IMEBADILISHA MAISHA YA MTEJA WETU