Home Burudani DIAMOND PLATNUMZ AFUNGUKA KUTAPELIWA BILIONI 4 ZA KUNUNUA NDEGE….ATAJA VIGOGO WA SERIKALI…

DIAMOND PLATNUMZ AFUNGUKA KUTAPELIWA BILIONI 4 ZA KUNUNUA NDEGE….ATAJA VIGOGO WA SERIKALI…

Diamond Plutnumz

Baada ya kutua Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga leo Oktoba 29, staa wa bongoflava Diamond Platnumz amefunguka kuhusu ishu ya ndege yake binafsi (private jet) aliyotaka kununua.

“Ishu ya ndege yangu ina mambo kidogo, nilinunua jet nimelipa fedha nimetapeliwa, nilimpigia Waziri Mbarawa (Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa) alinisaidia, kaka yangu Hamza ( Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari) alinisaidia na sasa serikali nzima inanisaidia kupata haki yangu, nililipa fedha nyingi, kianzio zaidi ya bilioni 4 ila niliowawatumia wananiletea ujanja ujanja,” amesema Diamond Platnumz

Diamond amekuwa akitumia ndege binafsi katika safari zake za ndani na nje ya nchi.

SOMA NA HII  KWA HALI HII YA SIMBA ROBERTINHO HANA MUDA MREFU