Home Habari za michezo AHMED ALLY :- GAMONDI ALIKUJA KUCHUKUA DARASA LA KUIFUNGA IHEFU JANA…

AHMED ALLY :- GAMONDI ALIKUJA KUCHUKUA DARASA LA KUIFUNGA IHEFU JANA…

Habari za Michezo

Ofisa Habari wa Klabu ya Simba Sc, Ahmed Ally amesema kuwa, Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi alikwenda jana kwenye Dimba la Mkapa kujifunza mbinu kutoka kwa watani zao Simba namna ya kumfunga Ihefu.

Ahmed amesema hayo wakati akizungumza na wanahabari baada ya mchezo wa jana wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Ihefu uliomalizika katika dimba la Mkapa kwa Simba kuibuka na ushindi wa bao 2-1.

Ikumbukwe kuwa, ndani ya Misimu miwili, Yanga imefungwa na Ihefu michezo yote ya ugenini na mchezo hivi karibuni Yanga ilipigwa bao 2-1.

Yanga ambayo inaongoza Ligi, mchezo ujao itakutana na mtani wake, Simba katika Dimba la Mkapa, hivyo kuna kila dalili kwamba Gamondi alikwenda kuwasoma wapinzani wake.

“Yanga alifanywa vibaya kwenye mashamba ya mpunga na Ihefu sasa isingekuwa uungwana kuliacha hili lipite hivi hivi, tumeamua kuwalipia Yanga Sc mabao waliofungwa na Ihefu (ambayo ni 2-1 ).

“Ndugu zetu tumewalipia kisasi mbabe wake tumemfanya vibaya na kocha wao (Miguel Gamondi) amekuja kwenye mechi yetu kujifunza na tunamuambia hii mechi ilikuwa ni ya mkakati wa kuchukua alama tatu kila mechi tunabadilika na Simba ya kwenye Derby itakuwa tofauti Uwanjani,” amesema Ahmed Ally.

SOMA NA HII  NYOTA HAWA WAWILI SIMBA KUWAKOSA WABOTSWANA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here