Home Habari za michezo MGUNDA:-“CHAMA HAYUPO SIMBA…HATUNA HAJA YA KUFICHA…AMEFUNGUKA HAYA

MGUNDA:-“CHAMA HAYUPO SIMBA…HATUNA HAJA YA KUFICHA…AMEFUNGUKA HAYA

Habari za Simba leo

kaimu Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Juma Mgunda amesema kuwa baadhi ya nyota wake akiwemo Clatous Chota Chama hawapo kwenye kikosi chake ambacho kitamenyana na Azam Fc kesho kutokana na majeruhi yanayowaandama.

Mgunda ambaye amechukua mikoba ya Benchikha amesema hayo leo wakati akizungumza kwenye mkutano na wanahabari kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Azam Fc.

Hivi karibuni Chama aliondoka nchini kwenda nyumbani kwao Zambia baada ya kupata majeraha lakini baadaye alifungiwa michezo mitatu na kamati ya nidhamu ya Bodi ya ligi kwa kumkanyaga Nickson Kibabage kwenye mchezo wa dabi dhidi ya Yanga.

“Mchezo wa soka ni mchezo wa wazi na wala hauna sababu ya kuficha. Ni kweli nina wachezaji majeruhi Chama ni majeruhi, ukiacha majeruhi ana adhabu ya kutumikia michezo mitatu na kesho utakuwa mchezo wa mwisho, lakini anaendelea vizuri.

“Wachezaji wengine ambao ni majeruhi ni Miquissone, Babacar na Saido. Onana naye alikuwa mejeruhi lakini ameanza mazoezi tangu jana.

“Simba SC imesajili wachezaji zaidi ya 30 ambao kazi yao ni kuitumikia klabu hii, kwa hiyo yoyote atakayepewa gwanda katika mchezo wa kesho atatimiza wajibu wake kwa sababu amesajiliwa

SOMA NA HII  SIMBA BADO KUNAFUKUTA MOTO...ZIMBWE JR AWAACHIA MSALA HUU WAZAWA