Home Habari za michezo KUELEKEA DABI YA KARIAKOO…JUA LA KESHO KUISHA NA MASTAA WA YANGA…SKUDU ATANGAZA...

KUELEKEA DABI YA KARIAKOO…JUA LA KESHO KUISHA NA MASTAA WA YANGA…SKUDU ATANGAZA RAHA ZAIDI…

Habari za Yanga

Kikosi cha Yanga SC, kesho Jumatatu, Oktoba 30, 2023 jioni kinatarajiwa kuanza mazoezi kuelekea Dabi ya Kariakoo.

Mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC ambao umepangwa kuchezwa Jumapili ijayo ya Novemba 5, 2023, tutakabiliana na Simba kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar Es Salaam.

Yanga tutaingia kwenye mchezo huo ikiwa vinara katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC tukifikisha pointi 18, huku tukifunga magoli 20 na kuruhusu magoli 4.

Katika hatua nyingine, Nyota wa kimataifa wa Klabu ya Yanga, raia wa Afrika Kusini, Skudu Makudubela, amewaahidi Wananchi kuwa watazidi kufurahi kila atakapokuwa anapewa nafasi.

Skudu ametoa kauli hiyo baada ya mchezo uliopita dhidi ya Singida Fountain Gate kuwapa raha Wanayanga kwa muda aliopewa nafasi ya kucheza kipindi cha pili, mchezo ambao ulimalizika kwa Yanga kushinda bao 2-0.

Kuhusu nafasi yake ndani kikosi, Skudu amesema: “Nitaweka juhudi kubwa katika uwanja wa mazoezi ili kumshawishi mwalimu anipe dakika za kutosha. Nawaahidi Wanayanga kuwa watazidi kufurahi kila nitakapokuwa napewa nafasi.”

Mchezo ujao wa Ligi utakuwa kati ya Yanga na Simba, Jumapili ijayo Oktoba 5, 2023 katika Dimba la Mkapa.

SOMA NA HII  BAADA YA KUMALIZANA NA WATATU CHAP....YANGA WAPANGA KUWAFANYIA 'UNYAMBISI' MASTAA WAKE WALIOBAKI...