Home Uncategorized HAWA NDIO WAPINZANI WA SIMBA KIMATAIFA HATUA YA AWALI

HAWA NDIO WAPINZANI WA SIMBA KIMATAIFA HATUA YA AWALI


WAPINZANI wa Simba kwenye michuano ya Kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika klabu ya UD Songo, imeanzishwa mwaka 1982 na kampuni moja kubwa nchini Msumbiji inayotambulika kwa jina la HCB, na ndilo jina la Uwanja ambao unaitwa Estadio da HCB.

Imezoea kucheza kwenye Uwanja wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 2,000 kama ilivyo Uwanja wao wa HCB.

Msimu uliopita US do Songo walishiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa waliishia hatua ya awali baada ya kutolewa na Nkana FC ya Zambia Kwa kufungwa mabao 3-1.


Watamenyana na Simba kati ya Agosti 9-11 wakiwa wenyeji wataifuata Simba mchezo wa marudio kati ya Agosti 23-25 Dar.

Mkononi wana kombe moja la ubingwa la Ligi ya Msumbiji maarufu kama Mocambola waliotwaa msimu wa 2017, kwa sasa ligi yao bado inaendelea.

SOMA NA HII  TANZANITE YAFANYA KWELI UGENINI, YAPINDUA MATOKEO KIBABE