Home Habari za michezo KUELEKEA ‘KARIKAOO DERBY’…BENCHIKHA AWAPA KISOMO MASTAA WOTE SIMBA…

KUELEKEA ‘KARIKAOO DERBY’…BENCHIKHA AWAPA KISOMO MASTAA WOTE SIMBA…

Habari za Simba leo

KUELEKEA mchezo wa Kariakoo Derby, Kocha Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha amefanya kikao kizito na wachezaji wake kwa kuyaweka mambo sawa kabla ya Aprili 20 mwaka huu.

Pambano la Kariakoo Derby linatarajiwa kuchezwa Aprili 20, mwak huu uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam ambapo Yanga wanakuwa wenyeji wa mchezo huo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Taarifa za uhakika zilizoifikia kutoka ndani ya bodi ya wakurugenzi Simba, kuwa baada ya kuondolewa katika kombe la CRBD Bank Federation na kupoteza alama mbele ya Singida Fountain Gate FC , viongozi, benchi la ufundi la wachezaji walikuwa na kikao.

Mtoa habari huyo amesema kikao hicho kilikuwa na ajenda mbili ikiwemo kushindwa kupata matokro lakini mipango ya kuelekea mchezo wa Derby ambao utafanyika Jumamosi hii baada ya mechi ya kwanza kupoteza kwa mabao 5 -1.

“Ni kweli baada ya kikao na viongozi kocha Benchikha (Abdelhak) alifanya kikao kingine na wachezaji wake tu bila ya kuwepo kwa kiongozi yoyote na kuzungumza nao na kuweka mipango yao kuelekea mechi dhidi ya Yanga.

Kocha hataki kupoteza mechi hiyo mara mbili n amewataka wachezaji kuwa makini ikiwemo safu ya ushambuliaji na ulinzi kutowapa nafasi ya wapinzani kufika katika eneo, lakini pia amerejesha morali ya wachezaji,” amesema chanzo hicho.

Mtoa habari huyo ameeleza kuwa timu hiyo inaweza kutoka nje ya Dar es Salaam kwa ajili ya kwenda sehemu kujichimbia kujiandaa na mchezo huo ambao wanahitaji pointi tatu kuliko chochote.

Naye Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa kazi kubwa ni kusak pointi tatu kwenye mechi ambazo wanachez ikiwa dhidi ya Yanga.

“Tunatambua kwamba tunamechi ngumu ambazo tunacheza hivyo tupo tayari kwa ajili ya kupata matokeo chanya mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi.

Wachezaji wapo tayari na wanatambua kwamba kila mchezo ni muhimu kwetu kupata ushindi, matokeo ambayo tunapata hayatufurahishi hivyo bado tunajipanga kupata matokeo,” amesema Ahmed .

SOMA NA HII  MASHINE MPYA YA MAGOLI SIMBA HII HAPA....KULIPWA MSHAHARA WA MIL 210 KWA MWAKA...