Home Habari za michezo ALLY KAMWE:- SIMBA NI TIMU TISHIO KWETU….WANAWACHEZAJI WENGI WAZOEFU…

ALLY KAMWE:- SIMBA NI TIMU TISHIO KWETU….WANAWACHEZAJI WENGI WAZOEFU…

Habari za Yanga leo

MSEMAJI wa Yanga Ali Kamwe amesema licha ya kupitia kipindi kigumu cha Simba, lakini wanaitazama timu hiyo katika mambo matatu muhimu kuelekea mchezo wa Derby utakaopigwa Jumamosi hii.

Kikosi kimerejea jana kutoka Mwanza na leo wanaingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo wa Kariakoo Derby, Yanga uwenyeji katika mchezo huo katika dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam saa 11:00.

Kamwe amesema anewataka mashabiki kuachana na fikra ya kuwa mpinzani wake amechoka na hajapata matokeo mazuri bali wanatakuwa kufikiri pointi tatu mbele ya Simba.

Amesema mechi ya Simba na Yanga ina umuhimu wake, huwa wakienda na mawazo ya mpinzania wao kuwa amechoka, hilo waliondoe na zaidi kutakiwa kuwa wanaenda kukutana na timu tishio.

“Hatuitazamani Simba kama wanavyotazama mashabiki bali ni timu tishio na tuko nao katika vita, kwa sababu wana wachezaji wazoefu wenye kucheza Derby kubwa na tofauti pia viongozi wa makini na wenye mipango na ubora wa hizi mechi,” amesema Kamwe.

Amewataka mashabiki wa Yanga, kuwa kujitokeza uwanjani na kuifanya Kariakoo Derby kuwa kilele cha siku ya Wananchi kwa kujaza uwanja na kutowapa nafasi ya wapinzani wao kuwa wengi.

“Asitokee mwanayanga akabaki nyumbani na baadae ya matokeo akajisifia, tunahitaji siku hizo kuwa ni kilele cha siku wananchi na tusiwape nafasi mashabiki wa pande wa pili kuwa wengi,” amesema Kamwe.

Kuhusu majeraha, amesema baadhi ya wachezaji wamerejea akiwemo Kennedy Musonda na Pacome Zouzoua yuko katika hatua nzuri ya kurejea katika hali yake ya kwaida.

“Hatuwezi kuwalazimisha wachezaji kucheza kwa sababu Yang ina kikosi kipana na tunaenda siku hiyo kwa roho ya kikatili,” amesema Kamwe.

Katika hatua nyingine Yanga kushirikiana na Bank ya NBC wamezindua kadi ya wanachama wa klabu hiyo ambayo itawasaidia katika mambo mbali mbali ikiwemo kuingia uwanjani.

Kwa munibu wa Rais wa Yanga, Hersi Said amesema Yanga inajivunia kuingia makubaliano na Bank bora ya NBC kwenda kuwahudumia wsnachama wetu kwenye usajili na kutoa kadi za uanachama.

Amesema Ukijiunga kuwa mwanachama wa Yanga na hapo hapo utapata huduma za kibenki , lakini kubwa zaidi kadi ya NBC imeungajishwa na huduma za N CARD hivyo mwanachama wetu atapata huduma ya kuingia uwanjani pamoja na huduma za usafiri

“Niwaombe pia benk ya NBC kutazama fursa nyingi zilizopo ndani ya klabu yetu tuna wanachama ndani na nje ya nchi na tunaimani Yanga ndio klabu sahihi ya kufanya nayo kazi kwenye sekta ya michezo na nyie ni mashahidi.

Tangu mdhamini Ligi Kuu Tanzania Bara , bingwa ni Yamga na niwahakikishie kama mtaongeza mkataba wa miaka 10 mbele, bado tutabaki kuwa bingwa katika kipindi chote,” amesema Hersi.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA