Home Habari za michezo VIFAA VIPYA MSIMBAZI HIVI HAPA…..NI MASHINE ZA KAZI HASWA….BENCHIKHA APIGA TIKI….

VIFAA VIPYA MSIMBAZI HIVI HAPA…..NI MASHINE ZA KAZI HASWA….BENCHIKHA APIGA TIKI….

Habari za Simba leo

WAKATI Simba ikijiandaa kwa ajili ya Derby dhidi ya Yanga Aprili 20, mwaka huu uwanja wa Benjamin Mkapa, uongozi wa Simba umeanza kuingia chimbo na kuanza kufanya usajili huku majina ya nyota watano yakiwa mezani mwa viongozi hao huku wanne wakigeni na mmoja mzawa.

Nyota hao wanaotajwa ni Chickna Diekite anacheza winga wa kushoto anayekipiga katika klabu ya Real Bamako ya nchini Mali, Derrick Fordjour kutoka klabu ya Medeama SC ya Ghana, mshambuliaji Foday Trawelly kutoka Brikama United na Rodger Torach kutoka klabu ya Vipers ya Uganda anacheza beki.

Simba imepeleka ofa kwa uongozi wa Singida Fountain Gate FC kuhitaji saini ya Nickson Kibabage ambaye anacheza Yanga kwa mkopo ambao unaisha mwishoni mwa msimu huu.

Taarifa kutoka ndani ya bodi ya wakurugenzi wa Simba, kuwa tayari majina hayo yapo mezani kwa ajili ya kujadiliwa ikiwa ni sehemu ya aina na nafasi ambazo zimependekezwa na Kocha Abdelhak Benchikha.

Chanzo cha habari kimesema kuna baadhi ya wachezaji ambao kocha anawahitaji kwa kutaja nafasi kazi kubwa imefanywa na skauti kuangalia aina ya wachezaji huku baadhi ya nyota wanatarajiwa kutemwa na wengine mikataba yao inamalizika.

“Kuna wachezaji ambao msimu ujao hawatakuea sehemu ikiwemo Saido Ntibazonkiza mkataba wake unafika ukingoni,Aubin Kramo huenda akaenda kwa mkopo Zesco ya Zambia na Henock Inonga yupo sokoni muda wowote anaweza kupigwa bei,” amesema chanzo hicho.

Ameongeza kuwa kabla ya msimu huo kumalizika Kocha Benchikha atakutana na Mwekezaji Mohammed Dewji (Mo) kwa ajili ya kufanya tathimini ikiwemo wachezaji watakaochwa na kuwaongeza kwa ajili ya msimu ujao.

Kwa mujibu wa Mwekezaji huyo kuwa atakutana na kocha huyo kwa ajili ya kujadili na kufanya tathimini ya timu yao na kuangalia nani wa kumtema na kuongeza kulingana na mapendekezo yake.

Katika hatua nyingine kocha Msaidizi wa Simba, Selema Matola amesema wana kazi kubwa ikiwemo safi ya ushambuliaji kutokuwa makini na nafasi wanazozipata.

Amesema wameumizwa kupoteza pointi mbili mbele ya Ihefu FC, kwa sababu wamecheza mpira mzuri na kumiliki mpira na kutengeneza nafasi lakini wameshindwa kuzitumia na kupoteza alama hizo.

“Tatizo letu like pale pale la kushindwa kutumia nafasi, ukiangalia Fred (Michael) angekuwa making tungepata matokeo, tunaenda kujiuliza na kufanyia kazi makosa hayo kujiamdaa na mchezo wetu dhidi ya Yanga.

Bado tupo katika mbio za ubingwa hatujakata tamaa na tunaenda kujipanga kwa ajili ya kusaka pointi tatu katika mchezo wetu wa Derby, naimani tutafanya vizuri,” amesema Matola.

Pambano la watani wa jadi linatarajia kuchezwa Aprili 20, mwaka huu huku Simba wakiwa ugenini katika dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI