Home Habari za michezo ZA NDAANI KABISAAA…HIZI HAPA SABABU ZA MOSES PHIRI KUPOTEANA SIMBA…BALEKE AONGEZA KITU..

ZA NDAANI KABISAAA…HIZI HAPA SABABU ZA MOSES PHIRI KUPOTEANA SIMBA…BALEKE AONGEZA KITU..

Habari za Simba

Kuna kipindi cha nyuma niliwahi kuwaambia mashabiki wa Simba sehemu fulani kuwa siku simba ikipata natural no 9(Namba 9 asilia) na akaingia kwenye mfumo vizuri basi Phiri atakaa benchi.

Ilikuwa ngumu kunielewa sababu Phiri alikuwa moto ila ndicho nilichagua kuamini. Kwa nini?

Kinachomfanya Phiri apate tabu kwenye soka letu ni kuwa muda mwingi anacheza kama play maker (mchezeshaji) na si finisher.

Soka letu la Tanzania linahitaji no 9 awe finisher zaidi kuliko kuwa play maker, yaani wewe uwe mkali kwenye kuweka mpira wavuni. Ndio maana Mayele anasemwa mchoyo ila anaufalme wake Yanga sababu anaweka Mpira wavuni.

Baleke anasemwa hana dribbling ability kubwa ila hajali yeye kila akiaminiwa na kocha anaweka Mpira wavuni ndio maana taratibu ameanza kujenga ufalme mpya kabisa pale simba.

Kama Baleke hatachuja basi inaweza kuwa mwisho wa zama nzuri za Moses Phiri pale Simba.

SOMA NA HII  HIKI HAPA KIKOSI KIZIMA CHA SIMBA KWA MSIMU HUU WA 2022/23...MASTAA HAWA NDIO WATAKAOPEPERUSHA BENDERA NYEKUNDU...