Home Habari za michezo YAMETIMIA….PABLO ATUPIWA VIRAGO SIMBA…MATOLA, BARBARA WATAJWA KUWA CHANZO…KOCHA MPYA NI HUYU HAPA…

YAMETIMIA….PABLO ATUPIWA VIRAGO SIMBA…MATOLA, BARBARA WATAJWA KUWA CHANZO…KOCHA MPYA NI HUYU HAPA…


Baada ya Msimu mbaya wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho kwa msimu wa 2021/2022, Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Klabu ya Simba Sports Club imevunja Mkataba na Kocha Mkuu wa Kikosi hicho Mhispaniola Pablo Franco na Kocha wa Viungo Daniel De Castro Reyes.

Katika Taarifa Rasmi iliyotolewa na Klabu ya Simba katika Mitandao yake ya Kijamii, leo Mei 31 imewashukuru walimu hao kwa michango yao wakati wa utumishi wao ndani ya Klabu.

Pablo aliwasili rasmi nchini Novemba 10, na amedumu ndani ya Kikosi cha Simba kwa miezi sita tu.

Pablo ameifikisha Simba SC Robo Fainali mbili, ambazo ni ile ya Kombe la Shirikisho Afrika na Kombe la Azam Sports Federation.

Itakumbukwa kuwa wakati Pablo anakuja nchini kuionoa Simba, wapenzi wa timu hiyo walitamba kuwa sasa soka maarufu la tiktaka la Barcelona litaanza kuchezwa Simba, hali ambayo imekuwa tofauti na matarajio ya wengi, kwani Simba imekuwa ikicheza soka la ‘butu butu butua’.

Hata hivyo, dalili za mahusiano ya kocha huyo na uongozi wa Simba kuwa mbaya zilianza kunyionyesha mapema kwenye mechi ya Pili ya Ligi Kuu baina ya Polisi Tanzania, mkoani Kilimanjaro, ambapo Pablo alikataa kusimamia mazoezi ya timu kwa kile alichodai kuwa hakuwa akipewa mazingira rafiki ya kufanya kazi, ikiwemo kupewa/kutafutiwa eneo zuri la timu kufanyia mazoezi.

Kutokana na msimamo huo, Kigogo wa juu wa Simba Alimlazimisha Pablo kwa njia ya Simu kusimamia mazoezi, jambo ambalo pia lalilikataa katu katu, hali ambayo Matola ambaye ni kocha Msaidizi alipewa amri ya kusimamia mazoezi.

Hali ilikuwa mbaya zaidi siku ya mechi, kwani tofauti na wengi walivyotarajio, Pablo alipanga kikosi dhaifu ambacho kilipelekea Simba kupata matokeo ya sare katika mechi hiyo muhimu ya kusaka alama tatu muhimu.

Timu iliporudi Dar, Pablo aliitwa ofisini ambapo inasemekana kuliibuka sintofahamu na kujibizana kati yake na Barbara Gonzalez, huku Pablo akiwataka Simba wampe barua ya kuvunja naye mkataba kisha wakutane kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la shirikiisho Afrika akiwa na timu nyingine.

SOMA NA HII  KUELEKEA SUPER LEAGUE....MPANGO WA MBRAZILI SIMBA KUMALIZANA NA AL AHLY UKO HIVI...

Hata hivyo, taarifa za ndani za timu hiyo kongwe nchini, pia zinasema kuwa Pablo alikuwa hapatani pia na msaidizi wake Selemani Matola, kwa kile alichokuwa akidai kuwa kocha huyo mzawa kuigawa timu na kutengeza mazingira magumu ya yeye kufanya kazi kama kocha Mkuu.

Pia sababu nyingine iliyopelekea Pablo kushindwa kufikia malengo ndani ya Simba, ni kutokana na kushindwa kuitawala timu na wachezaji, kwani mara kadhaa wachezaji wakongwe na wenye majina makubwa walikuwa wakimuonyesha dharau za wazi,huku kukiwa hakuna kalipio lolote kutoka kwenye utawala wa Klabu.

Kuondoka kwa Pablo, kunaweka wazi nafasi ya Kocha Mkuu, klabuni hapo, ambapo taarifa za uhakika zinadai kuwa Kocha wa Zamani wa Waydad Casablanca ya Morocco Mohammed Adil Erradi tayari yupo nchini muda mrefu kumalizana na Simba kwa ajili ya kupewa kibarua cha kuiona timu hiyo.

Kocha huyo mwenye haiba na wajihi sawa na aliyekuwa Kocha wa Simba, Mfaransa Didier Gomez, hivi sasa ni Kocha Mkuu wa APR ya Rwanda, ametua Tanzania hivi karibuni huku akifanya mazungumzo mengi na Simba ya namna ya kukiboresha kikosi hiko.


Soma kwa Kirefu hapa chini, Taarifa ya Klabu ya Simba.