Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA WAARABU…MASTAA WOTE YANGA KUPIGWA CHINI….GAMONDI AFUNGUKA HILI..

KUELEKEA MECHI NA WAARABU…MASTAA WOTE YANGA KUPIGWA CHINI….GAMONDI AFUNGUKA HILI..

Yanga SC

LICHA ya mastaa wengine wakiwa katika majukumu ya timu za taifa, Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema anatarajia kufanya mabadiliko ya kikosi chake katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria.

Kikosi cha Yanga kinaendelea na maandalizi ya mchezo huo watakuwa ugenini Novemba 24, mwaka huu katika dimba la Stade du Juillet nchini humo kuhakikisha wanaendeleza ubabe wao wa kusaka matokeo chanya.

Gamondi amesema anamatarajio ya kuingia katika mcheso huo kwa mbinu nyingine ikiwemo kufanya mabadiliko ya kikosi kwa sababu anaimani ya CR Belouizdad nao wamekuwa wakiwafatilia tangu makundi yalipopangwa.

Amesema licha ya wao kuwafatilia CR Belouizdad katika michezo yao, pia Yanga wamekuwa wakifatiliwa kwa umakini na kuhakikisha anafanya mabadiliko ya kikosi katika mchezo huo wa ugenini.

“Mabadiliko ya kikosi yatakuwepo, wachezaji watakapokamilika wote kila mmoja atakuwa anajua majukumu yake, katika mchezo huo hatutaingia kama ilivyo kwa michezo mingine tuliocheza awali,” amesema Gamondi.

Ameongeza kuwa yuko makini na kuimarisha kikosi katika kila sekta ikiwemo ushambuliaji ambao tayari amefanyia kazi na kuendelea na safu ya ulinzi kulingana na uimara wa washambuliaji wa CR Belouizdad.

“Nimewafatilia baadhi ya michezo yao ambayo wakicheza nayo wamefanikiwa kufunga bao kila mechi, hilo tuko nalo makini kuhakikisha haturuhusu bao. Kufikia huko lazima tujiweke sawa kila eneo na kuwakumbusha mabeki kuwa makini.

Kikosi kipo vizuri licha ya wachezaji wengine kuwepo kwenye majuku ya timu zao za taifa waliobaki wanafanya kazi majukumu yao tujiweke imara zaidi ya mechi zilizopita,” amesema kocha huyo

Amesisitiza kuwa wamejiandaa kwa mapambano ya aina yote kila mchezaji kufanya kazi kwa ushirikiana mkubwa ili kufikia malengo wsnayoyatarajia kwa msimu huu.

Kocha huyo amesema anachohitaji ni kupata ushindi katika mchezo wa kwanza, anaamini akianza vizuri haitokuwa kazi kubwa kwenye michezo inayofuata.

Wachezaji wa timu hiyo walipata mapumziko ya siku moja na kesho (jumatatu),wanarejea kwenye uwanja wa mazoezi kuendelea na maandalizi ya mchezo huo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa mara ya kwanza kucheza hatua hiyo.

SOMA NA HII  MSIGWA ATABIRI MAKUBWA YANGA...ITAFIKA LEVEL ZA MAN UTD, ARSENAL