Home Uncategorized AKITUA HUYU JANGWANI, ENEO LA KATI VITA YA NAMBA ITAKUWA SI MCHEZO

AKITUA HUYU JANGWANI, ENEO LA KATI VITA YA NAMBA ITAKUWA SI MCHEZO


SALUM Abubakar,’Sure Boy’ kiungo anayekipiga ndani ya Azam FC iwapo dili lake la kutua Yanga litajibu basi itaongeza vita ya namba.

Kwa sasa Yanga ina viungo watano ambao wanacheza kati ikiwa ni pamoja na Haruna Niyonzima, Feisal Salum Fei Toto’, Issa Mohammed ‘Banka’, Papy Tshishimbi na Mapinduzi Balama ‘Kipenseli.

Habari zinaeleza kuwa Yanga ipo kwenye hesabu za kukamilisha dili la nyota huyo kutua mitaa ya Jangwani jambo litakaloongeza upana wa kikosi na ushindani wa namba eneo la kati.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa mpango wa kuboresha kikosi upo ila itategemea na mahitaji ya Kocha Mkuu, Luc Eymael.

SOMA NA HII  UTAMU WA LIGI YA MABINGWA HUU HAPA NA MERIDIAN BET