Home Uncategorized YANGA YAIPIGA MKWARA AZAM FC, NYOTA WAO HUYU MMOJA KUKOSEKANA

YANGA YAIPIGA MKWARA AZAM FC, NYOTA WAO HUYU MMOJA KUKOSEKANA


 LEO Novemba 25, Yanga itakuwa Uwanja wa Azam Compex kusaka pointi tatu dhidi ya Azam FC mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku wakiweka wazi kwamba wanahitaji pointi tatu.


Mchezo wa leo unakuwa ni wa kwanza kwa mzunguko wa kwanza kwa vigogo hawa ambao wapo ndani ya tatu bora baada ya kucheza mechi 11 za Ligi Kuu Bara.


Azam FC ni vinara wakiwa wameizidi idadi ya mabao matano Yanga kwa kuwa safu ya ushambuliaji ya Azam FC inayoongozwa na Prince Dube imefunga mabao 18 huku ile ya Yanga inayoongozwa na Michael Sarpong imefunga mabao 13 wote wana pointi 25.


Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa nyota wao Mapinduzi Balama ataukosa mchezo wa leo kwa kuwa bado hajawa fiti ila wachezaji wengine wapo sawa.


“Tumekamilisha kila kitu kilichobaki ni kukamilisha kazi uwanjani ya kupata pointi tatu muhimu hilo lipo wazi na tutapambana kufanya vizuri.


“Mwalimu amenihakikishia kwamba kila kitu kipo sawa na tutaweza kupata ushindi kwenye mchezo wetu dhidi ya Azam FC, hatuna shida na Ice Cream sijui, ukwaju hayo tunawaachia wao sisi tunataka pointi tatu muhimu,” amesema.

SOMA NA HII  SIMBA YATOSHANA NGUVU NA AFRICAN SPORTS