Home Habari za michezo ZA NDANII KABISA…MECHI SIMBA NA YANGA…MAREFA HAWA WOTE WANAWAKE

ZA NDANII KABISA…MECHI SIMBA NA YANGA…MAREFA HAWA WOTE WANAWAKE

ZA NDANII KABISA...MECHI SIMBA NA YANGA...MAREFA WOTE WANAWAKE

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya mchezo wa dabi kuonekana safu nzima ya waamuzi kuwa jinsi ya kike kuhakikisha dakika 90 zinamalizika salama.

Inadaiwa kuwa kamati ya waamuzi ilishamaliza kuteua majina ya waamuzi hao kitambo sana tena wote wenye hadhi ya Fifa lakini kutokana na ukubwa wa mchezo kuna safu nyingine ya watu wanatakiwa kuwekwa.

Chanzo kutoka kamati ya waamuzi kinaeleza wao walishamaliza kazi yao ya kuteua majina kisha kuyawakilisha TFF kwa ajili ya mambo mengine ikiwa pamoja na kuyatangaza.

“Majina yote ya waamuzi nayafahamu lakini kimaadili siwezi kukutajia japo tulitarajia hadi muda huu yangekuwa yametangazwa hivyo sijui kinachokwamisha maana huu ni mchezo mkubwa,” kinaeleza chanzo hicho.

Chanzo kingine kutoka ndani zaidi kinadai mwamuzi wa kati atasimama, Jonesia Rukyaa, wamuzi wa pembeni yupo, Janeth Balama na mmoja kati ya Zawadi Yusuph na Glory Tesha kama hakutakuwa na mabadiliko.

Waamuzi wa akiba (official) anaweza akawa, Tatu Malogo au Ester Adalbert lakini tayari lugha gongani imeanza kujitokeza huko ndani.

“Kuna wengine walitaka, Tatu ndio asimame kati lakini Jonesia ndio anaonekana kukubalika zaidi, ugumu unakuja kati ya Zawadi pamoja na Glory hapo ndio kuna mgawanyiko nani apewe nafasi.” anasema mtoa taarifa.

Hata hivyo anasema majina ya waamuzi yatatangazwa muda wowote kuanzia leo Ijumaa, Aprili 14 baada ya taratibu nyingine kukamilika.

SOMA NA HII  SIMBA KUWAFUATA BIASHARA UNITED LEO