Home Habari za michezo SIKU ZA JOB ZAHESABIKA YANGA…AGOMA KUSAINI MKATABA MPYA…UTATA MZITO WAIBUKA

SIKU ZA JOB ZAHESABIKA YANGA…AGOMA KUSAINI MKATABA MPYA…UTATA MZITO WAIBUKA

SIKU ZA JOB ZAHESABIKA YANGA...AGOMA KUSAINI MKATABA MPYA...UTATA MZITO WAIBUKA

UGUMU wa beki wa kati wa Yanga, Dickson Job kushindwa kusaini mkataba mpya hadi sasa ni ishu ya mshahara anaoutaka na siyo dau la usajili kama ilivyokuwa awali.

Mwanzoni ilisemekana Yanga walitaka kumpa beki huyo mkataba na Sh70 milioni ili kusaini, lakini yeye akataka Sh100 milioni na hivyo jambo hilo kukwama kabla ya sasa kuibuka lingine.

Ipo hivi; uongozi wa Yanga hautaki yajirudie ya Feisal Salum ‘Fei Toto’ kwenye ishu ya masilahi na sasa nyota huyo haichezei timu hiyo licha ya kuwa ni mchezaji wao halali.

Job ambaye ameonyesha kiwango kikubwa tangu asajiliwe na miamba hiyo akitokea Mtibwa Sugar (2021/22) mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu na amekuwa akizuvutia timu nyingi zinazohitaji huduma yake.

Hata hivyo, pamoja na mabingwa hao watetezi wa Ligio Kuu Bara kumwongezea mshahara kutoka Sh4milioni hadi 6 milioni, nyota huyo ameweka ngumu na anataka ufike Sh10 milioni, jambo linaloleta ugumu kwa mabosi wa Yanga kuendelea kumshawishi kusalia ndani ya kikosi hicho.

Habari kutoka kwa mmoja wa kiongozi wa timu hiyo, zinasema Yanga haina shida kumpa dau la usajili la 100 milioni Job, ishu ni kwenye mshahara anaoutaka wa Sh10 milioni ambao wanaona kila mzawa akiutaka kuna eneo wanaweza wakakwama.

“Ugumu wa kumbakiza Job utakuwepo kwenye mshahara anaotaka na wana umoja wa kuambiana mishahara yao, sasa kila mzawa akimaliza mkataba wake na akawa anataka pesa hizo tutazitoa wapi? ukizingatia pesa tunategemea kwa GSM siku akiondoka itakuaje;

Aliongeza “Tunajua zipo timu zinazozungumza naye kuhusu kutaka huduma yake, ndio maana tukafanya jitihada ya kumwongeza angalau kutoka Sh4 hadi 6 milioni, ili kumwonyesha tunathamini kiwango chake.

“Kuhusu wageni wanalipwa pesa nyingi, ukiona hawaonyeshi kiwango inatokea ni upepo mbaya kwao, kwa sababu tunapowachukua kwenye timu zao wanakuwa kwenye kiwango cha juu sana, tofauti na wengi wanavyodhani.”

Hilo ni kama limempa alamu kocha wa timu hiyo, Nasreddine Nabi kuanza kumtumia Ibrahim Abdallah Hamad ‘Bacca’ ili lolote litakalotokea mwishoni mwa msimu kikosi chake kiwe salama.

“Kocha Nabi anajua kuyasoma mazingira ya wachezaji na hataki kikosi chake kiyumbe, mfano namna anavyoliziba pengo la Fei Toto kupitia kwa Mudathir Yahya, ndio maana kwa sasa ameanza kumpa nafasi ya mara kwa mara Bacca ili kikosi chake kisije kikayumba,”alisema.

Ingawa Nabi mwenyewe aliwahi kufafanua sababu ya kumtumia Bacca mechi dhidi ya US Monastir kwamba ilitokana na vimo virefu vya wapinzani wao na aliweza kucheza vizuri.

Hata hivyo, SOKA LA BONGO lilimtafuta meneja wa beki huyo, George Job ili azungumzie kuhusiana na mkataba wa mteja wake alifafanua

“Mazungumzo kwa sasa yanaendelea vizuri, ingawa siwezi kufafanua sana hadi itakapofika wakati sahihi kila kitu kitakuwa wazi, sitaki kutaja na timu anaweza kwenda au vinginevyo lakini nafikiri jambo zuri tusubiri muda sahihi.”

SOMA NA HII  HUYU HAPA KIUNGO PUNDA SIMBA...ACHUKUA TUZO YA MCHEZAJI BORA