Home Habari za michezo FT: DODOMA JIJI 0-2 YANGA SC….AMBUNDO ‘AWAMBUNDUA’ MABOSI ZAKE…YANGA BADO NNE WAITWE...

FT: DODOMA JIJI 0-2 YANGA SC….AMBUNDO ‘AWAMBUNDUA’ MABOSI ZAKE…YANGA BADO NNE WAITWE BINGWA…


BAADA ya kucheza mechi tatu bila kupata ushindi hatimaye vinara Yanga wameng’ara ugenini kwa kuichapa Dodoma jiji Mabao 2-0 mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Yanga walianza mpira kwa kushambulia kwa kasi yake na katika dakika ya 11 Dickson Ambundo aliwanyanyua mashabiki wake baada ya kufunga bao nzuri kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Dodoma.

Licha ya kupata bao Yanga waliendelea kulishambulia lango la wenyeji na mnamo dakika ya 35 Golikipa wa Dodoma jiji Mohammed Yusuph alijifunga baada ya shuti la Zawadi Mauya.

Mnamo dakika ya 87 Dodoma jiji walipata pigo baada ya kiungo wake Hassan Maulid kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kumchezea rafu Yannick Bangala.

Kwa ushindi huo Yanga wamefikisha Pointi 60 wakiwa wanahitaji Pointi 11 waweze kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu wakiwa wamebakiwa na Mechi 6 mkononi nafasi ya pili wapo Simba wakiwa na Pointi 49 huku wakiwa wamebakiwa mechi 7.

SOMA NA HII  AHAMED ALLY AWEKA WAZI KILICHOMPELEKA GAMONDI KWENYE MECHI YA SIMBA JANA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here