Home Michezo ALI KAMWE:_ STRAIKA WAO ANAPIGA KICHWA KAMA KONDOO…YANGA VS US MONASTIR NI...

ALI KAMWE:_ STRAIKA WAO ANAPIGA KICHWA KAMA KONDOO…YANGA VS US MONASTIR NI FUNDISHO

Afisa Habari wa Yanga SC Ally Kamwe

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kikosi cha timu hiyo kimetoa somo namna ya kuzifunga timu kutoka Kaskazini mwa Afrika (Waarabu).

Kamwe ametoa kauli hiyo baada ya Yanga kuitungua US Monastir ya Tunisia kwa bao 2-0 katika Dimba la Mkapa na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

“Yanga tumetoa somo zuri ya jinsi gani ya kumfunga mwarabu nyumbani kwako. Kama kuna timu inataka kuchukua hili somo download mechi yetu dhidi ya Monastir kisha utanikumbuka baadae.

“Hakikisha mnapoangalia na nyie mna striker kama Musonda, kama striker wako anapiga kichwa kama kondoo usijishuhhulishe kuangalia,” amesema Kamwe.

Ikumbukwe pia kuwa, Yanga iliifunga Clube Africain ya Tunisia katika hatua ya mtoano na kufanikiwa kutinga hatua ya Makundi ya Kombe hilo.

SOMA NA HII  CHAMA AWACHAMBUA WACHAMBUZI WA SOKA...MFUNGAJI BORA WA MUDA WOTE CAF