Home Uncategorized YANGA YAANZA KUSUKA KIKOSI KAZI CHA KUIMALIZA SIMBA NOVEMBA 7

YANGA YAANZA KUSUKA KIKOSI KAZI CHA KUIMALIZA SIMBA NOVEMBA 7


 KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze, anataka kukibadilisha kikosi chake hicho kabla ya kuwavaa wapinzani wao Simba, Novemba 7.

 

Katika mkakati huo, viongozi wa Yanga wamependekeza kwa Kaze kuwa asafiri na wachezaji wake wote waende Kanda ya Ziwa kwa ajili ya mechi dhidi ya Biashara United na Gwambina ili amtathmini mchezaji mmoja mmoja kabla ya kupata kikosi kitakachoivaa Simba.


Yanga jana Oktoba 22 ilicheza na Polisi Tanzania jijini Dar na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na baada ya hapo itaivaa Biashara Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Karume, Musoma kabla ya kupambana na Gwambina kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Novemba 3.


Yanga ambayo ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, inajipanga kuhakikisha inafanikiwa kutwaa ubingwa chini ya kocha Kaze ambaye ameanza kukinoa kikosi hicho hivi karibuni.


Habari zinaeleza kuwa, kutokana na kocha kuwa na muda mchache na kikosi hicho, ameutaka uongozi kuhakikisha nyota wote wanapata nafasi ya kusafiri na timu katika mechi za mikoani ili kupata nafasi ya kumuangalia kila mchezaji na kupata kikosi cha kwanza kitakachoivaa Simba.


“Mwalimu amewataka wachezaji wote wajitume na wajitoe katika kuipambania timu yao ili kuweza kupata matokeo mazuri katika kila mechi watakayocheza kwa kila mmoja kutambua jukumu lake lililomleta Yanga.

 

“Pia kutokana na muda kutotosha, ameuomba uongozi kuhakikisha kila mchezaji anakuwa katika sehemu ya safari ya timu hiyo katika mechi za mikoani ili kupata nafasi ya kumuangalia mchezaji mmoja mmoja akiwa anaendelea kusaka kikosi chake cha kwanza kabla ya kuivaa Simba.

 

“Kwanza amewataka wachezaji kuhakikisha wanajituma na kupata matokeo mazuri katika kila mechi wanayocheza kwa kuwa kila aliyetua Yanga ni bora pamoja na kuibuka na pointi tatu katika mechi zote tatu watakazocheza kabla ya kuivaa Simba,” alisema mtoa taarifa huyo.

 Ofisa Habari wa timu hiyo, Hassan Bumbuli, alithibitisha: “Ni kweli waliopendekeza ni uongozi baada ya kuona kocha ana muda mfupi wa kukaa na timu ikiwa zimebaki siku 11 kabla ya kukutana na Simba, tumeona akiondoka na wachezaji wachache, wengine hatawaona katika muda huo mfupi wa siku zilizobakia, hivyo amekubaliana na uongozi wa kwenda na wachezaji wote, mwenyewe amefurahi ili apate muda wa kuweza kuwaona wachezaji wote kabla ya mechi yetu na watani na atakayebakia ni Mapinduzi (Balama) tu.” 

SOMA NA HII  VPL:POLISI TANZANIA 0-0 YANGA


Chanzo:Championi