Home Habari za michezo KISA KAKOLANYA KUTOKUCHEZESHWA…JULIO AWALIPUA SIMBA…” HAIWEZI KUWA TIMU BORA NI UOGA”….

KISA KAKOLANYA KUTOKUCHEZESHWA…JULIO AWALIPUA SIMBA…” HAIWEZI KUWA TIMU BORA NI UOGA”….


Kocha Msaidizi wa timu ya Namungo, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema ni uoga kwa timu ya Simba kumtumia kipa mmoja msimu mzima huku wakijiita wao ni timu kubwa.

Akifanyiwa mahojiano na Sport Arena ya Wasafi FM, Julio amesema; “Mimi kama mwalimu, Philosophy yangu siwezi kumtumia golikipa mmoja lakini huo ni uoga.

“Kwa sababu makipa wengine hawawaamini,Beno Kakolanya hata kwenye ligi ya nyumbani anacheza pale ambapo Manula ana matatizo labda ya kadi au anaumwa lakini kinyume Cha hapo hawezi kucheza.

“Hiyo haiwezi kuwa Timu bora au Timu yenye kikosi kipana ambacho wenyewe wanajinasibu unapokuwa na kikosi kipana mtu yeyote anapaswa acheze.

“Huyu akikosekana hakuna doubt lakini ukisema Aishi hayupo, Simba tunafeli, Aishi ni kipa bora kwa mchango wake anaisaidia Simba 75% ya kufika hapa walipofika,” amesema Julio.

SOMA NA HII  SIKU CHACHE BAADA YA MBRAZILI KUSEPA...MGUNDA ASHUSHA PRESHA SIMBA...