Home Habari za michezo BAADA YA KUTUA TU SAUZI…SIMBA WALIA HUJUMA…HIVI NDIVYO BALOZI WA TZ...

BAADA YA KUTUA TU SAUZI…SIMBA WALIA HUJUMA…HIVI NDIVYO BALOZI WA TZ ALIVYOWAOKOA….


Msafara wa viongozi pamoja na wachezaji wa Simba leo wamewasili salama nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao dhidi ya Orlando Pirates ila wamebainisha kwamba mapokezi yalikuwa ni mabaya.

Ikiwa inanolewa na Kocha Mkuu,Pablo Franco ina kazi ya kusaka ushindi Aprili 24 kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali ya pili itakayoamua matokeo ya timu itakayotinga hatua ya nusu fainali, Kombe la Shirikisho Afrika.

Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa Simba wameachia ujumbe huu:”Asanteni Orlando Pirates kwa mapokezi mazuri lakini mmetunyima Polisi wa kutoongoza barabarani,(escorti) hivyo tumelazimika kutumia gari la Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini kutuongoza,”.

Ni Meja Jenerali Gaudence Milanzi ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini ameweza kuweka wazi kwamba kwa upande wa ulinzi na usalama ni wa kutosha hivyo wawakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa wasiwe na mashaka wacheze mpira.

Kwenye mchezo huo Simba inahitaji ushindi wa aina yoyote ama sare ili kuweza kutinga hatua ya nusu fainali ubaya ni kwamba ikiwa itafungwa kwenye mchezo huo itafungashiwa virago mazima.

Tazama msafara wa Simba hapa chini wakielekea Hotelini;

???? Asanteni Orlando Pirates kwa mapokezi lakini mmetunyima polisi wa kutuongoza barabarani (escort) hivyo tumelazimika kutumia gari la Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini kutuongoza. #NguvuMoja pic.twitter.com/fZDdRbnnGP

— Simba Sports Club (@SimbaSCTanzania) April 22, 2022

SOMA NA HII  BAADA YA KUISASAMBUA IHEFU JANA...MBRAZILI SIMBA ATAJA MKAKATI WA KUMALIZANA NA YANGA...