Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA KESHO DHIDI YA NAMUNGO…NTIBAZONKIZA KUKOSEKANIKA…SABABU HII HAPA…

KUELEKEA MECHI YA KESHO DHIDI YA NAMUNGO…NTIBAZONKIZA KUKOSEKANIKA…SABABU HII HAPA…


Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amethibitisha kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo Saido Ntibazonkiza atakosekana kwenye mchezo wa dhidi ya Namungo utaopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa kutokana na majeraha.

Akiongea na waandishi wa habari kocha Kaze amesema Saido hawezi kuwa sehemu ya kikosi hicho lakini anamini urejeo wa viungo waliokuwa majeruhi kama Khalid Aucho na Feisal Salum β€˜Fei Toto’ tayari watasaidia timu katika mchezo huo.

”Tunatambua ni mchezo mgumu lakini tumejipanga kuondoka na alama tatu ili kujiweka katika mazingira kabla ya kuwavaa watani zetu Simba wiki ijayo” amesema Kaze.

Yanga wanakutana na Namungo katika mchezo wa mzunguko wa 20 wakiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya bao 1-1 katika pambano la kwanza lililopigwa katika uwanja wa Ilulu mkoani Lindi.

SOMA NA HII  VIDEO: ISHU YA MANJI KUREJEA YANGA, MASHABIKI WAFUNGUKA