Home kimataifa GRIEZMANN AIBEBA UFARANSA IKIBANWA MBAVU EURO

GRIEZMANN AIBEBA UFARANSA IKIBANWA MBAVU EURO


 STAA wa timu ya taifa ya Ufaransa Antoine Griezman amefanikiwa kuibeba timu yake baada ya kufunga bao la kusawazisha dhidi ya Hungary katika sare ya kufungana bao 1-1.

Katika mchezo huo Hungary ndiyo walikuwa wa kwanza kucheka na nyavu dakika ya 45 kupitia kwa nyota wao Attila Fiola na kuwafanya waende mapumziko wakiwa kifua mbele.

N Griezmann ambaye alipachika bao la kuweza usawa dakika ya 66 na kufanya ngoma ikamilike kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Ikumbukwe kwamba katika michuano ya Euro 2016 Griezaman alikuwa mfungaji bora baada ya kufunga mabao 6 na Ufaransa ilipoteza kwenye mchezo wa fainali kwa kufungwa na Ureno ambao walisepa na taji hilo.

SOMA NA HII  TAJIRIKA 'CHAP' NA MACHAGUO SPESHO YENYE ODDS KUBWA KUBWA KUTOKA MERIDIANBET...