Home Yanga SC NYOTA SITA WA YANGA KUIKOSA MWADUI LEO KWA MKAPA

NYOTA SITA WA YANGA KUIKOSA MWADUI LEO KWA MKAPA


WAKATI leo Juni 20 kikosi cha Yanga kinatarajiwa kushuka Uwanja wa Mkapa kusaka pointi tatu dhidi ya Mwadui FC, kuna hatihati ya kuwakosa nyota sita kutokana na sababu mbalimbali. 

Nyota hao ni Metacha Mnata kipa namba moja wa Yanga huyu amesimamishwa kutokana na utovu wa nidhamu kwa muda usiojulikana.

Farid Mussa, Mukoko Tonombe hawa bado hawajawa fiti baada ya kupata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Lamine Moro nahodha wa Yanga, Michael Sarpong na Wazir Junior hawapo kwenye mpango wa Nabi.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wao uliopita walipokutana Uwanja wa Kambarage, ubao ulisoma Mwadui 0-5 Yanga.

Kwenye msimamo Yanga ipo nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 30 kibindoni ina pointi 64 inakutana na Mwadui FC ambayo ipo nafasi ya 18 na pointi 19.

SOMA NA HII  YANGA vs CLUB AFRICAIN:...FANYEENI YOOTEE LAKINI HILI LA MWAMUZI MKILISAHAU IMEKULA KWENU....