Home Yanga SC KASEKE, FEI TOTO WAWEKA REKODI YAO KWA MKAPA

KASEKE, FEI TOTO WAWEKA REKODI YAO KWA MKAPA


 VIUNGO wawili wa Klabu ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi Feisal Salum na Deus Kaseke, Juni 17 waliweka rekodi yao Uwanja wa Mkapa kwa kuhusika kwenye mabao yote matatu ambayo yalifungwa na timu hiyo.


Wakati ubao ukisoma Ruvu Shooting 2-3 Yanga, ni miguso ya wazawa hao ilihusika katika mabao hayo yaliyowapa pointi tatu mazima Yanga.

Bao la kwanza ambalo lilifungwa na Feisal dakika ya 22 kwa pasi ya Mrundi, Fiston Abdulazak na bao la pili lilifungwa na Fei kwa pasi ya Kaseke dakika ya 32.

Pia Kaseke alisababisha faulo dakika ya 77 baada ya kuchezewa na Mohamed Banka nje kidogo ya 18 ambapo ilijazwa kimiani na Saido Ntibanzokiza dakika ya 79.

Katika mchezo huo wazawa hao waliweza kutimiza majukumu yao kwa kupambana kwa ajili ya timu hiyo kupata pointi tatu na walifanikisha lengo hilo kwa ushirikiano wa pamoja na wachezaji wenzao.

SOMA NA HII  KISA KUWA MFUNGAJI BORA CAF....SIFA ZAZIDI KUMIMINIKA KWA MAYELE....STAA MKUBWA MALI AMPA MAUA YAKE...