Home kimataifa JEZI YA MESSI YAOGOPWA BARCELONA

JEZI YA MESSI YAOGOPWA BARCELONA


IMEELEZWA kuwa jezi namba 10 ndani ya kikosi cha Barcelona wengi wanaigwaya kwa sasa kutokana na rekodi ambazo aliziweka mwamba huyo ambaye kwa sasa yupo ndani ya kikosi cha PSG.

Jezi hiyo kwenye kikosi hicho kwa sasa ipo wazi hakuna ambaye anaivaa baada ya Messi kusepa mazima ndani ya miamba hiyo ya La Liga.

Aliyekuwa anapewa nafasi ya kuvaa jezi hiyo alikuwa ni mshikaji wake wa karibu Kun Aguero ambaye naye aliikacha jezi hiyo.

Aguero ambaye aliibuka hapo akiwa mchezaji huru akitokea Manchester City na alitarajia kucheza kwa ukaribu na Messi ndoto yake imemeguka amechagua jezi namba 19.

Mwandishi mmoja nchini Hispania alinukuliwa akisema kwamba hakuna ambaye ataenda kuvaa jezi namba 10, hakuna ambaye anaushajaa wa kuvaa jezi hiyo.

SOMA NA HII  BAADA YA KUCHAPWA JUZI...KOCHA MAN UTD AJA NA STAILI MPYA YA KUJITETEA...AWASHUSHIA LAWAMA MASTAA ...