Home Habari za michezo KISA KADI TANO ZA NJANO JANA….TFF WAFUNGUKA ISHU YA SIMBA KUSHUSHIWA RUNGU...

KISA KADI TANO ZA NJANO JANA….TFF WAFUNGUKA ISHU YA SIMBA KUSHUSHIWA RUNGU LA ADHABU…

Simba haitaadhibiwa na Bodi ya Ligi kwa wachezaji wake kuonyeshwa kadi tano za njano kwenye Dabi ya Kariakoo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Sheria, Habari na Masoko wa TFF, Boniface Wambura. Adhabu itatolewa iwapo timu itapata zaidi ya kadi tano za njano.

Katika mchezo wa jana Jumapili, Oktoba 23 2022, Derby ya Kariakoo, klabu ya Simba SC imepata kadi za njano tano huku watani wao wa jadi, klabu ya Yanga SC ikipata kadi za Njano nne (4).

Mwamuzi wa mchezo, Ramadhani Kayoko ametoa kadi za njano 9 kama ifuatavyo;

Okra Augustine (Simba)
Feisal Salum (Yanga)
Mzamiru Yassin (Simba)
Mohamed Hussein (Simba)
Khalid Aucho (Yanga)
Tuisila Kisinda Aziz Ki (Yanga)
Djuma Shabani (Yanga)
Habib Kyombo (Simba).

Mpaka kipenga cha mwisho, timu zote zimetoshana nguvu kwa kutoka sare ya kufungana bao 1-1. Simba ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Augustine Okrah dakika 15 kabla ya Aziz Ki kuisawazishia Yanga kwa mkwaju wa adhabu dakika ya 45 ya

SOMA NA HII  MORRISON AENDELEA KUKIWASHA YANGA...VITUKO NA MANJONJO YAKE VYAZIDI KUWA KEROO..