Home Uncategorized NYOTA KANE ANAWINDWA NA MANCHESTER UNITED

NYOTA KANE ANAWINDWA NA MANCHESTER UNITED


MSHAMBULIAJI wa Spurs, Harry Kane amesema kuwa anahitaji kupata changamoto mpya kwa sasa nje ya timu yake hiyo anayoitumikia.
Spurs imekuwa kwenye mvutano mkubwa na nyota huyo ambaye inaelezwa kuwa hafurahii maisha ndani ya kikosi hicho kutokana na kuona kwamba hakina nafasi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England.
Manchester United iliyo chini ya Kocha Mkuu Ole Gunnar Solskjaer inatajwa kuwania saini yake ili kumpata nyota huyo aishi ndani ya Old Trafford.
Kibiashara inatajwa kuibeba Manchester United kutokana na uwezo wa Kane ambaye ni nyota anayekipiga ndani ya timu ya Taifa ya England akiwa ni nahodha pia.

SOMA NA HII  ISHU YA USAJILI, YOUTUBE HAKUNA MCHEZAJI MBAYA, TIMU ZA BONGO ZIBADILIKE