Home Uncategorized CHELSEA YATEMBEZA KICHAPO KWA RENNERS LIGI YA MABINGWA ULAYA

CHELSEA YATEMBEZA KICHAPO KWA RENNERS LIGI YA MABINGWA ULAYA

 

KLABU ya Chelsea, usiku wa kuamkia leo imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Renners.

Olivier Giroud, nyota wa Cheksea alipachika bao la ushindi dakika za usiku kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Renners ikikubali kichapo cha 1-2.


Callum Hudson Odoi alianza kupachika bao dakika ya 22 ambalo lilipinduliwa na Serhou Guirassy dakika ya 85 zikiwa zimebaki dakika tano ngoma kukamilika Uwanja wa Stade de la Route de Lorient. 


Ushindi huo unaifanya Chelsea kushika uskani wa kundi E baada ya kufikisha jumla ya pointi 10 wakibebwa na idadi ya mabao ya kufunga ambapo wamefunga mabao 9 wakifuatiwa na Sevilla ambao wamefunga mabao 6.


Timu zote hizi mbili kwenye mechi nne, zimeshinda tatu na kukusanya sare mojamoja na kuwa na pointi 10 kibindoni. 


Kwa upande wa mashuti ambayo yaliyolenga lango kwa timu zote idadi ni sawa ambapo kila timu ilipiga jumla ya mashuti matano, kwa Chelsea mawili yalileta mabao huku kwa wenyeji Renners shuti moja likimshinda kipa namba moja Edouardo Mendy raia wa Ufaransa.

SOMA NA HII  ARUSHA FC YAIPIGIA HESABU KALI GIPCO