Home Uncategorized COASTAL WASEPA NA POINTI TATU ZA IHEFU, MABAO 7 YA SIMBA YANAWATESA

COASTAL WASEPA NA POINTI TATU ZA IHEFU, MABAO 7 YA SIMBA YANAWATESA


 JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa mabao 7-0 waliyopata mbele ya ya Simba bado yapo kwenye vichwa vyao jambo ambalo linamfanya apate muda wa kukaa nao ili waweze kufanya vizuri kwenye mechi zao zijazo.


Bao pekee la Coastal Union lilipachikwa kimiani na nahodha Salum Ally dakika 16 akiwa nje ya 18 kwa guu lake la kulia lililomshinda mlinda mlango namba moja wa Ihefu, Isihaka Joseph.

Mchezo wa Ihefu uliopita walilazimisha sare ya bila kufungana na Polisi Tanzania, Uwanja wa Azam Complex na leo wamekubali kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Mgunda amesema:”Vijana wamepambana kwa kadri ya uwezo ila naona kwamba licha ya kupata ushindi bado wanashindwa kurekebisha makosa yao, yale makosa yao yanajirudiarudia hasa ya mchezo uliopita.


“Ambacho nitakifanya ni kukaa nao chini kuzungumza ili kuweza kutoa makosa yale yaliyopita ili kuona namna gani tutaweza kuwa bora, bado nafasi ipo na tunaamini tutafanya vizuri,” .

SOMA NA HII  VIDEO; SAKATA LA CHAMA KUHAMIA YANGA LIPO NA MAAMUZI YA TFF