Home Uncategorized MANCHESTER UNITED YATEMBEZA 4G, YAKIOA KISASI

MANCHESTER UNITED YATEMBEZA 4G, YAKIOA KISASI

 


Usiku wa kuamkia leo Manchester United imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Instanbul Basaksehir katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. 


Watupiaji kwa Manchester United ni Bruno Fernandes alitupia mawili, dk ya 7 na 19, Marcus Rashford alitupia bao moja kwa penalti dakika ya 35 na msumari wa mwisho ni Daniel James dakika ya 90+2.


Lile lla Instanbul Basaksehir ndani ya Uwanja wa Old Trafford lilipachikwa dakika ya 75 na Deniz Turuc ni Kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.


Manchester United ikiwa kundi H ni vinara wakiwa na pointi 9 kibindoni na Insanbul ipo nafasi ya nne na pointi 3 ambazo ilizipata kwa United baada ya ushindi wa mabao 2-1,Novemba 11 Uwanja wa Basaksehir Fatih Terim.

SOMA NA HII  KUMEKUCHA. YANGA, SIMBA KUSAJILI KWA FAINI