Home EURO 2020 MBAPPE AKWAMISHA NDOTO ZA UFARANSA KUTINGA HATUA YA ROBO FAINALI

MBAPPE AKWAMISHA NDOTO ZA UFARANSA KUTINGA HATUA YA ROBO FAINALI


KYLIAN Mbappe nyota wa timu ya taifa ya Ufaransa penalti yake ilikwama kuzama nyavuni mbele ya timu ya taifa ya Switzerland katika mchezo wa hatua ya 16 bora Euro 2020.


Nyota huyo alipiga penalti ya 10 iliweza kukutana na mikono ya kipa wa Switzerland Yann Sommer ambaye alikuwa nyota wa mchezo huo umewafanya Ufaransa waweze kuishia hatua hiyo kwa kufungwa jumla ya penalti 5-4 kwa kuwa dk 90 ngoma ilikamilika 3-3 licha ya kwamba walikuwa wanapewa nafasi ya kushinda.

Alikuwa ni Haris Seferovic aliyeanza kupachika bao kwa upande wa Switzerland kwa kichwa dk 15 na lingine dk ya 81 huku lile la tatu likipachikwa dk 90 na Mario Gavranovi kwa Ufaransa ni Karim Benzema yeye alipachika mabao mawili dk ya 57 na 59 na bao moja alipachika Paul Pogba kwa shuti kali akiwa nje ya 18 likazama kimiani mazima. 

SOMA NA HII  VIDEO: MASHINDANO YA EURO YAWAPAGAWISHA MASHABIKI