Home Uncategorized MALENGO YA BIASHARA UNITED NI TANO BORA, YAWAOMBA WADAU KUIPA SAPOTI

MALENGO YA BIASHARA UNITED NI TANO BORA, YAWAOMBA WADAU KUIPA SAPOTI


SELEMAN Mataso, Mwenyekiti wa Klabu ya Biashara United amesema kuwa mipango mikubwa iliyo ndani ya klabu hiyo ni kupambana kumaliza ligi ikiwa ndani ya tano bora.


Akizungumza na Saleh Jembe, Mataso amesema kuwa kwa sasa timu imeshaanza maandalizi ya kuelekea mchezo wao dhidi ya Ndanda FC utakaochezwa Nangwanda Sijaona.

“Tupo vizuri tunajiandaa na mechi zetu zilizobaki ila kikubwa ni kwamba bado tunahitaji sapoti kutoka kwa wadau ili kufanikisha malengo ambayo tumejiwekea ikiwa ni pamoja na kumaliza ligi tukiwa ndani ya tano bora.

“Mchezo wetu dhidi ya Ndanda FC utakuwa mgumu ila kuna gharama ambazo zinahitajika kukamilisha safari yetu ninaomba wadau wasichoke kuwa nasi bega kwa bega katika hili,” amesema.

Biashara United ipo nafasi ya 10 ikiwa imecheza mechi 29 na kibindoni ina pointi 40.
SOMA NA HII  MSIMAMO WA LIGI KUU BARA BAADA YA MNYAMA KUTULIZWA TAIFA