Home Yanga SC YANGA WATAJA SIKU YA KUCHUKUA UBINGWA WA LIGI KUU BARA

YANGA WATAJA SIKU YA KUCHUKUA UBINGWA WA LIGI KUU BARA


 HASSAN Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa ni suala la muda tu kwa timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara huku wakitaja siku ya kuchukua ubingwa.

Yanga ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi zake 70 baada ya kucheza mechi 32 huku Simba ambao ni mabingwa watetezi wakiwa nafasi ya kwanza na wana pointi 73.

Bumbuli amesema kuwa kwa namna yoyote ile wao ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimu huu na hilo litakuwa wazi baada ya wao kumaliza mechi zao mbili ambazo zimebaki.

Bumbuli amesema :-“Wakibahatisha safari hii wakibahatisha kushinda, wakachukua hapa itakuwa ni bahati yao. Kwanza huu msimu sisi mabingwa niulize kuanzia tarehe 13 mwezi huu wa 7. Mpaka tarehe 23 mwezi wa saba tutakuwa mabingwa.

“Tuna mechi mbili zimebaki ambazo ni dhidi ya Ihefu na Dodoma Jiji, baada ya kumaliza mechi hizo hapo mtajua kwamba nani anakuwa bingwa, sisi hatuna wasiwasi na ubingwa maana hawana namna ya kuweza kuchukua ubingwa,” amesema Bumbuli.

 Chanzo:Azam TV

SOMA NA HII  KWA HILI GAMONDI KAZI ANAYO HUKO YANGA