Home Habari za michezo KWA HILI GAMONDI KAZI ANAYO HUKO YANGA

KWA HILI GAMONDI KAZI ANAYO HUKO YANGA

Habari za Yanga SC

Hakuna kitu kizuri kama kuiangalia Yanga ya Gamondi ikicheza, kama unadaiwa kodi, una njaa, una uchovu ama unaumwa homa ndogondogo basi ni dawa inayotibu kwa dakika 90 tulizoshuhudia pale Azam Complex, Chamanzi.

Hakuna kitu kigumu hivi sasa kama kutabiri kikosi cha Yanga kitakachoanza, kila mchezaji anapata nafasi na anakupa kile unachohitaji kwa ubora wa hali ya juu.

Hakuna kitu kigumu kama kutaja man of the match kwenye mchezo wa leo kutokana na namna wachezaji wote walivyomwaga jasho kuipigania bendera ya kijani na njano.

Sio Kibwana aliyekosa michezo kadhaa, sio Mkude aliyekua Morogoro kwenye mechi mbili za nyuma, sio Sure boy aliyekaa benchi mechi mbili, sio Max , sio Kibabage, sio Pacoume aliyeingia kutokea Sub, sio Azizi ki aliyezaliwa upya msimu huu, wala sio Mzize ambaye hakuwepo hata sub kwenye mchezo uliopita kila mmoja anakiwasha.

Hapo bado man of the match kwenye mchezo dhidi ya KMC, Mudathir yuko benchi mtawala wa dimba la kati Doctor Khalid Aucho yuko jukwaani, Yao Attouhoula, Lomalisa, Kenedy Musonda.

Beki bora wa Ligi msimu uliopita na captain kwenye mchezo dhidi ya KMC Dickson Job wanaitazama mechi kwenye TV na bado Asas kala Mkono na mpira mwingi.

Hakuna mtihani mgumu kama kuwa Gamondi, uanze na mchezaji yupi na yupi akae benchi, kila anayepata nafasi anacheza.

Hakuna kitu kigumu kama kukabiliana na ile pressing ya Yanga kuanzia highline, kutoka dakika ya kwanza mpaka 90, wanakuja tu kama wana ugomvi.

SOMA NA HII  AUCHO AFUNGIWA MECHI TATU,REFA COASTAL UNION NA YANGA WAHUSISHWA NJE NUSU MWAKA