Home Uncategorized FILAMU YA NDEMLA WA SIMBA KUPELEKA MKATABA WAKE YANGA HII HAPA

FILAMU YA NDEMLA WA SIMBA KUPELEKA MKATABA WAKE YANGA HII HAPA

INAELEZWA kuwa Simba imempatia kiungo wake, Said Ndemla mkataba mpya ili aendelee kusalia klabuni hapo baada ya ule wa awali kuelekea ukingoni taarifa nyingine zinadai Ndemla ameuchukua mkataba huo na kuupeleka Yanga akiwataka waboreshe maslahi ili aichezee timu hiyo.
Ndemla amekuwa akihusishwa kuhamia Yanga msimu ujao baada ya kukaa kwa muda mrefu ndani ya Simba huku akionekana kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara.
  
Habari za kuamini zinasema mkataba aliopewa Ndemla na Simba una maelewano ya kumpatia Sh milioni 30 ili aendelee kusalia klabuni hapo.

“Kuna uwezekano mkubwa sana kwa Yanga kuuchana mkataba wa Simba ambao wamempa Ndemla hivi karibuni kama tu watafikia kiasi cha shilingi milioni 45 ambazo Ndemla amewataka wampatie kama kweli wanahitaji huduma yake msimu ujao.
“Unajua Simba wamemuwekea ofa ya Sh milioni 30, fedha ambazo wanataka aongeze mkataba wa miaka miwili, lakini Yanga wao wanataka kumpatia Sh milioni 40 asaini hiyo miaka miwili kikosini kwao.
“Lakini wanaomsimamia Ndemla wamewataka Yanga watoe Sh milioni 50 au 45 endapo kweli wanamtaka na walitaka fedha hiyo iwe kwa mwaka mmoja jambo ambalo Yanga nao wameomba muda kabla ya kufikia siku ya Ijumaa ambayo Ndemla anatakiwa kuwasilisha jibu sahihi kule Simba.
“Kwa maana hiyo, kama Yanga watakubaliana na watu wa upande wa Ndemla, basi kiungo huyo atasaini Yanga kwa kipengele cha kucheza kikosi cha kwanza,” kilisema chanzo hicho.
Alipotafutwa Ndemla mwenyewe kuzungumzia ishu hiyo, hakupatikana, lakini upande wa Yanga kupitia kwa Ofisa Mhamasishaji na Msemaji wa klabu hiyo, Antonio Nugaz, alisema: “Hivi sasa masuala hayo yote ambayo unayasikia kuhusu sijui usajili na mambo mengine yapo kwenye hatua za mwisho katika kujadiliwa na uongozi, mambo yakiwa fresh tutaweka hadharani kila kitu,”. 

Hivi karibuni, Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck, alizungumzia nafasi ya Ndemla ndani ya Simba na kumtaka aonyeshe juhudi ili acheze, huku akiongeza kuwa, kama kuna mchezaji wake anataka kuondoka, anamruhusu.

Chanzo: SpotiXtra
SOMA NA HII  NYOTA WA MWADUI AIYEE AWAAMBIA YANGA WAPELEKE MKWANJA MREFU