Home Uncategorized MTIBWA SUGAR HAWANA HESABU ZA KUKAA MEZANI KUZUNGUMZIA OFA ZA WACHEZAJI

MTIBWA SUGAR HAWANA HESABU ZA KUKAA MEZANI KUZUNGUMZIA OFA ZA WACHEZAJI



UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa kwa sasa hauna mpango wa kuzungumzia ofa za wachezaji wake kutokana na kuwekeza nguvu nyingi kupambana na Virusi vya Corona.


Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa ni ngumu kuwa huru kuzungumza kuhusu kuuza wachezaji kwa wakati huu wa janga la Corona.

“Kila mtu anapenda kitu kizuri na Mtibwa Sugar ni moja nya sehemu ambayo ina wachezaji wengi wazuri na wana uwezo mkubwa ila hatuna muda wa kuzungumza kuhusu kuwauza.

“Nguvu kubwa kwa sasa ni kwenye mapambano dhidi ya Virusi vya Corona ninapenda kila mmoja awe makini na achukue tahadhari, tumewaambia wachezaji wawe mabalozi wazuri wakati huu wa hili janga,” amesema.

Miongonin mwa wachezaji wanaopigiwa hesabu na timu mbalimbali ni pamoja na Dikcson Job, Shomari Kibwana, Jaffary Kibaya.
SOMA NA HII  SHIME AWAPA TANO WACHEZAJI KUICHAPA UGANDA, MASHABIKI WAHUSIKA