Home Uncategorized NI MSALA MWINGINE YANGA, SERIKALI YAMPIGA STOP BALAMA, SABABU ZATOLEWA

NI MSALA MWINGINE YANGA, SERIKALI YAMPIGA STOP BALAMA, SABABU ZATOLEWA


IDARA ya Uhamiaji Tanzania imemzuia kiungo mshambuliaji mpya wa Yanga, Mapinduzi Balama kujiunga na kambi ya kujiandaa na mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga imeingia kambini Jumanne ya wiki hii huko Chuo cha Mwika Wildlife kilichopo Moshi, Kilimanjaro ambako inajiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Township Rollers ya Botswana.

Timu hizo zinatarajiwa kucheza mchezo huo wa marudiano Agosti 24, mwaka huko Botswana baada ya awali kutoka sare ya kufungana bao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Mratibu wa timu hiyo, Hafidh Saleh amesema kuwa, kiungo huyo aliachwa Dar kwa ajili kukamilisha kibali cha kusafiria kinachosimamiwa na Idara ya Uhamiaji.

“Balama yupo njiani, hapa ninavyozungumza na wewe, tulishindwa kuja naye ili akamilishe hati yake ya kusafiria.

“Ilikuwa lazima tumuache Dar ili ajiunge na wenzake baada ya kocha kuutaka uongozi ukamilishe haraka hati yake ya kusafiria tayari kwa safari ya Botswana.

“Hivyo, Balama yupo njiani kuja kujiunga na wenzake kambini hapa Moshi ambako tutacheza mchezo mmoja wa kirafiki na Polisi Tanzania na baadaye AFC Leopards ya nchini Kenya huko Arusha,” alisema Hafidh.

SOMA NA HII  MSIMAMO WA LIGI KUU BARA UPO NAMNA HII