Home news KUHUSU KIWANGO CHAKE KUSHUKA…FEI TOTO AVUNJA UKIMYA YANGA…AMNYOOSHEA KIDOLE NABI…

KUHUSU KIWANGO CHAKE KUSHUKA…FEI TOTO AVUNJA UKIMYA YANGA…AMNYOOSHEA KIDOLE NABI…


KIUNGO fundi wa mpira anayekipiga Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amevunja ukimya baada ya kuwa nje ya uwanja kutokana na majeraha akiwatoa hofu mashabiki wa klabu hiyo kuwa bado kidogo awarejeshee utamu.

Kulikuwa na taarifa kwamba huenda Fei Toto angekuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya mwezi mmoja tangu alipoumia kwenye mechi dhidi ya Coastal Union, lakini amesema kwa sasa anaendelea vyema na tayari amejiunga na wenzake kambini.

Fei Toto aliyekosa mechi mbili – moja ya Ligi Kuu dhidi ya Polisi Tanzania na nyingine ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Mbao, alisema amerejea kikosini kwa vile ana maendeleo mazuri kiafya na kumfanya sasa aungane na wenzake.

“Naendelea vizuri ndio maana nipo na wenzangu kambini tukiendelea na ratiba nyingine zote, jambo ambalo limenifanya kuingia katika mpango wa mechi ya leo dhidi ya Mbeya City,” alisema Fei Toto.

“Nipo fiti na tayari kucheza mechi hiyo labda itokee kocha (Nasreddine Nabi) asinipange kwa mchezo huo na ligi. Ila naamini katika utimamu wangu wa mwili nikirejea uwanjani baada ya kukosekana nitakuwa na kiwango kama cha awali.”

Fei Toto alisema mashabiki wa Yanga na wote wanaotamani kumuona uwanjani akicheza wasiwe na wasiwasi wowote, kwani yupo vizuri kuipigania timu hiyo ili kutimiza malengo yao.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA MAMBO MAGUMU KWA WAARABU...ADEBAYOR AANZA KUJISOGEZA SIMBA KIAINA...