Home Habari za michezo ROBERTINHO AKIACHA KIKOSI CHA SIMBA KAMBINI ATIMKIA BRAZIL

ROBERTINHO AKIACHA KIKOSI CHA SIMBA KAMBINI ATIMKIA BRAZIL

Habari za Simba SC

KAMBI ya Simba iliyopo hoteli ya Latapya, jijini Ankara Uturuki inazidi kunoga kwa wachezaji kuanza kuchangamshwa kwa mazoezi ya aina mbalimbali ikiwamo ya kuogelea ili kusaka pumzi, lakini kocha mkuu wa timu hiyo, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ametimka ili kwenda darasani.

Simba ipo nchini humo kujiandaa na msimu mpya wa mashindano ikitarajiwa kucheza mechi zisizopungua tatu kabla ya kuja kuwasha moto kwenye Tamasha la Simba Day itakayofanyika Agosti 6 kisha kwenda kucheza mechi za Ngao ya Jamii kufungulia msimu mpya wa Ligi Kuu Bara itakayoanza Agosti 15 kisha kuanza jukumu la mechi za kimataifa za CAF litakaloanza Agosti 18.

Hata hivyo, kwa sasa mastaa waliopo Ankara kwa sasa wakati wanawasubiri wenzao akiwamo Jean Baleke na wapya waliosajiliwa hivi karibuni akiwamo Willy Onana, Che Fondoh Malone kuungana nao, watakuwa chini ya makocha wasaidizi baada ya Robertinho kurudi darasani kuboresha cv yake.

Chanzo cha kuaminika kutoka kambi hiyo ya Simba, kimeeleza kuwa, Robertinho ameondoka akiwaaaga wachezaji wake kuwa anakwenda kusoma kwa muda kabla ya kuunganao nao tena baadaye kwa ajili ya kuanza msimu mpya wa mashindano.

β€œSina taarifa kamili anaenda kusomea nini, ila ninachokifahamu ni kwamba ameondoka kwenda kusoma na programu za mazoezi ya maandalizi ya timu hiyo kwa sasa, amemuachia kocha msaidizi kutoka Burundi na wenzake walipo hapa,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;

β€œTimu inaendelea na mazoezi kama ilivyopangwa kocha ameacha program zote tuta kuwa na mechi za kirafiki kama alivyoomba.”

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Robertinho kurudi darasani baada ya Januari 30 mwaka huu kuposti picha zikimuonyesha yupo darasani nchini kwao Brazili na kuiacha timu chini ya aliyekuwa msaidizi wake, Juma Mgunda ambaye inaelezwa kwa sasa hatakuwa na kikosi hicho tena.

soka la bongo liliwasiliana na Robertinho ili atoe ufafanuzi kwa kile anachoenda kukisoma kwa sasa, lakini hakukuwa na majibu kwani simu yake kwa njia ya whatsapp, ilikuwa ikiita bila kupokelewa na ujumbe mfupi wa maneno alisoma tu bila kujibu.

SOMA NA HII  KIRAKA MPYA WA YANGA APEWA MITIHANI MITATU CHAP