Home Michezo KOCHA GEITA GOLD:- WALETENI HAO YANGA…TUNAAPA KULIPA KISASI

KOCHA GEITA GOLD:- WALETENI HAO YANGA…TUNAAPA KULIPA KISASI

KOCHA GEITA GOLD:- WALETENI HAO YANGA...WAMEAPA KULIPA KIISASI

BAADA ya kupangwa na Yanga, kocha mkuu wa Geita Gold, Fredy Felix ‘Minziro’ amesema kabla ya droo kuchezeshwa alijiandaa kisaikolojia kuikabili timu yoyote atakayopangiwa na baada ya kukabidhiwa Wanajangwani atajipanga zaidi ili asirudie makosa japo amekiri kuwa haitakuwa rahisi.

Geita Gold wametumia dakika 180 kwenye Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga na kupoteza michezo yote miwili kwa kufungwa mabao 4-1 baada ya mchezo wa awali kukubali kichapo cha bao 1-0 na mzunguko wa pili kuchapwa 3-1.

Akizungumza na Nasi, Minziro alisema taarifa za kukutana na Yanga zilikuwa ni suprizi kwake kwasababu hakujua atakutana na timu gani lakini baada ya kusikia ratiba hiyo alisema ana dakika 90 nyingine ngumu kumkabili bingwa mtetezi wa Kombe la Shirikisho la Azam (FA).

“Tumetoka kumalizana naye kwenye ligi, tulifanya makosa kwa kukubali kipigo cha mabao 3-1. Kitendo cha kupangwa naye tena FA tunahitaji kufanya kazi kubwa kuhakikisha haturudii makosa na kuzitumia dakika 90 vyema ili kuvuka hatua nyingine ya mashindano hayo.”

SOMA NA HII  UNAAMBIWA PAMOJA NA KUWA KASEPA SIMBA....BALEKE BADO NI MWEKUNDU TU...ISHU IKO HIVI...