Home Yanga SC HAJI MANARA ANA NONGWA NA SIMBA, AFUNGUKA MAPYA KUHUSU BILIONI 20 ZA...

HAJI MANARA ANA NONGWA NA SIMBA, AFUNGUKA MAPYA KUHUSU BILIONI 20 ZA DEWJI


HAJI Manara, usajili mpya ndani ya Yanga katika kitengo cha habari ameweka wazi kuwa yeye hana kisasi  ila ana nongwa ya kahawa huku akigusia dili la mzigo wa bilioni 20 za Simba.

Manara alitambulishwa ndani ya Yanga, Agosti 24 mbele ya Waandishi wa Habari na kukabidhiwa jezi ya Yanga na kazi yake ya kwanza ilikuwa ni Agosti 25, Mlimani City ambapo alitambulisha jezi mpya za Yanga.

Akiwa ndani ya Simba aliweza kudumu kwa muda wa miaka sita alikuwa ni Mkuu wa Kitengo cha Habari alisepa ndani ya kikosi hicho baada ya kuwaaga mabosi wake kupitia kundi la Simba HQ na taarifa rasmi ya kusepa kwake Simba ilitolewa Agosti 28.

Manara amesema:”Mimi kisasi sina ila nina nongwa ya kahawa. Kahawa kikombe chake kidogo kinaunguza, hiyo ni sifa yake mbaya, pili ya moto, tatu siku hizi wanaongeza pilipili mtama, tangawizi , sijui mavitu gani hii ni sifa mbaya nina nongwa ya kizaramo haiishi.

“Sitawafanyia nongwa Simba, siwezi kama wenyewe wanavyojinasibu kuwa Simba ni kubwa kuliko mtu yoyote.  Mimi nina nongwa kwa sababu nilitumia nguvu kubwa kuibrand timu ile na kuwaaminisha watu yasiyowezekana na mengine yaliwezekana.

“Kwa mfano baada ya sakata lile siku tatu mbele ikatengenezwa press, (Mkutano) kunitoa njiani mimi ikatengenezwa press na bango kubwa likawekwa. Tusiongopeane ile ni taasisi kubwa, unasema umeweka bilioni 20, benki gani?

Katika mkutano huo unaozunguziwa ni cheki ya bilioni 20 ambayo ilisainiwa ikiwa ni sehemu ya uwekezaji ndani ya kikosi hicho.


SOMA NA HII  BAADA YA KICHAPO CHA SIMBA...NABI AFUNGUKA HAYA..AMTAJA AZIZ KI