Home Uncategorized SASA MECHI KUPIGWA KAMA KAWAIDA, NYUMBANI NA UGENINI, VITUO HAKUNA

SASA MECHI KUPIGWA KAMA KAWAIDA, NYUMBANI NA UGENINI, VITUO HAKUNA


RASMI sasa mechi zote zitachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini bila kuwepo vituo kama ambavyo awali ilielekezwa.

Dr. Hassan Abass, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema kuwa suala hilo limezingatia maoni ya Wizara ya Afya pamoja na wadau mbalimbali wa masuala ya michezo.

“Serikali imeridhia mfumo wa michezo ya soka uchezwe kama ilivyokuwa ukifanyika awali, yaani kwa mfumo wa nyumbani na ugenini, kabla ya Virusi vya Corona.

“Awali ilipangwa ichezwa kwa vituo na ilitokana na kuwepo kwa Virusi vya Corona lakini kwa kuwa hali inazidi kuwa shwari na Serikali imeridhia kuwe na mechi za nyumbani na ugenini kwa kila mechi ili kutoa burudani na furaha iendelee vilevile.

“Jambo la msingi ni kuona kwamba utaratibu unafuatwa ikiwa ni pamoja na kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona kwani licha ya kwamba hali imekuwa shwari lakini ni lazima kuchukua tahadhari,”.

Vituo ambavyo vilipangwa awali ilikuwa ni kwa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho kituo cha Dar es Salaam na zile za Ligi Daraja la Kwanza na la Pili zingechezwa Mwanza.

Hii ilikuwa ni kutokana na kuchukua tahadhari dhidi ya janga la Virusi vya Corona ambalo linaivuruga dunia.

Ligi inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 13 huku ratiba ikitarajiwa kutolewa leo, Mei 31.

SOMA NA HII  ALGERIA BINGWA MPYA WA AFRIKA, AMNYOOSHA SENEGAL KIDOGO TU