Home Michezo MAYANGA ATENGENEZEWA UFALME MITBWA SUGAR…KOCHA ATHIBITISHA

MAYANGA ATENGENEZEWA UFALME MITBWA SUGAR…KOCHA ATHIBITISHA

MAYANGA ATENGENEZEWA UFALME MITBWA SUGAR...KOCHA ATHIBITISHA

MSHAMBULIJI wa Mtibwa Sugar, Vitalis Mayanga amesema licha ya kuanza taratibu na kikosi hicho ila mashabiki wake watarajie makubwa zaidi.

Nyota huyo alijiunga na timu hiyo katika dirisha dogo la Januari akitokea kwa Maafande wa Polisi Tanzania na kufunga bao moja tu dhidi ya Dodoma Jiji Februari 11, mwaka huu na kufikisha mabao matatu ya Ligi Kuu Bara.

“Bado ninahitaji muda zaidi wa kuendelea kuelewana na wachezaji wenzangu kwa sababu kule nilikotoka tayari nilishatengeneza muunganiko mzuri ingawa taratibu kuna kitu kinaanza kuonekana kwangu,” alisema na kuongeza;

“Licha ya ufalme nilioutengeneza nikiwa Polisi ila sikuogopa kuondoka na kutafuta changamoto sehemu nyingine nikiamini ili niwe bora ni lazima nijue namna ya kuishi maisha tofauti na yale niliyoyazoea mwanzoni.”

Kwa upande wa Kocha Msaidizi wa Mtibwa Sugar, Awadh Juma ‘Maniche’ alisema tangu usajili wa mchezaji huyo ndani ya kikosi chao umekuwa na manufaa makubwa kwani hata ushindani umeongezeka zaidi tofauti na mwanzoni.

“Unapokuwa na wachezaji bora zaidi ya wawili katika nafasi moja basi ni lazima ushindani utakuwepo tu kwani kila mmoja atataka kucheza, sasa hali kama hii ni nzuri kwenye timu kwa sababu ni njia ya kufanya vizuri.”

SOMA NA HII  RAJA CASABLANCA 3-1 SIMBA SC...ONYANGO AICHOMESHA SIMBA MOROCCO