Home news ‘KWA YANGA HII YA MAYELE, ‘FEI TOTO’ MOLOKO, AUCHO…HATA WAJE LIVERPOOL HAWATOKI...

‘KWA YANGA HII YA MAYELE, ‘FEI TOTO’ MOLOKO, AUCHO…HATA WAJE LIVERPOOL HAWATOKI KWA MKAPA’…


BAO la kipindi cha kwanza la mshambuliaji Fiston Mayele dakika ya 36, na lile la kipindi cha pili la Jesus Moloko dakika ya 70, yametosha kuipa Yanga pointi tatu muhimu dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Yanga ilianza kipindi cha pili kwa kushambulia lango la Azam FC kama walivyoanza mchezo katika kipindi cha kwanza huku umakini kwa washambulia wao Fiston Mayele na Yacouba Sogne ukikosekana baada ya kukosa nafasi kadhaa za kufunga.

Dakika ya 60, kiungo wa Azam FC Sospeter Bajana alikuwa mchezaji wa kwanza kwenye mchezo huu kupata kadi ya njano baada ya kumchezea madhambi winga mshambuliaji wa Yanga Jesus Moloko.

Azam ilijaribu kufanya mashamhulizi kadhaa ya kutaka kusawazisha bao hilo ila jitihada hizo ziligonga mwamba kutokana na uimara unaoendelea kuonyeshwa na safu ya ulinzi ya Yanga.

Licha ya George Lwandamina kufanya mabadiliko Dakika ya 67, kwa kuwaingiza Ayoub Lyanga na Idris Mbombo  ili kuongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji ila hawakuweza kuleta madhara yeyote mbele ya mabeki wa Yanga.

 jitihada hizo hazikuweza kufanikiwa mbele ya safu ya ulinzi ya Yanga ambapo dakika ya 70, ilifanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa winga Jesus Moloko na kuendelea kupata matokeo ya ushindi bila ya kuruhusu nyavu zao kuguswa msimu huu.

Dakika ya 73, Yanga ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa Yacouba Sogne na Jesus Moloko huku nafasi zao zikichukuliwa na Farid Musa na Yusuf Athuman.

Dakika ya 85, Azam ilifanya mabadiliko kwa kumtoa Never Tigere na nafasi yake kuchukuliwa na Frank Domayo.

Huku kwa upande wa Yanga wakimtoa Feisal Salum ‘Fei Toto’ na nafasi yake ikichukuliwa na Mukoko Tonombe.

Kipigo hichi kwa Azam kinakuwa cha pili msimu huu baada ya Oktoba 2, kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania.

Kwa matokeo haya Yanga inaendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa kufikisha pointi 12, huku Azam ikisaliwa na Pointi nne ikiwa nafasi ya 11, baada ya timu zote kucheza michezo minne.

SOMA NA HII  BOCCO KUONGOZA MASHAMBULIZIDHIDI YA JWANENG..KIKOSI KAMILI HIKI HAPA...