Home Habari za michezo PAMOJA NA KUICHARANGA KMC KWA HASIRA JUZI…MATOLA ASHINDWA KUJIZUIA KWA ALICHOKIONA…ADAI WALISUMBUA…

PAMOJA NA KUICHARANGA KMC KWA HASIRA JUZI…MATOLA ASHINDWA KUJIZUIA KWA ALICHOKIONA…ADAI WALISUMBUA…


Kaimu Kocha Mkuu, Seleman Matola, amesema ushindi walioupata jana dhidi ya KMC walistahili kutokana na kiwango kikubwa kilichooneshwa na wachezaji wake. Matola amesema timu yake ilicheza vizuri muda wote na wachezaji walijitahidi kufuata maelekezo aliyowapa.

Matola ameongeza kuwa, kipindi cha kwanza KMC waliingia kwa njia ya kuzuia hivyo wote wakawa nyuma ya mpira lakini kipindi cha pili walivyofunguka waliweza kuwafunga.

“Ukiangalia mchezo mzima sisi tulikuwa bora zaidi yao, tulitengeneza nafasi nyingi na tulistahili kupata ushindi kwa kuwa tulicheza vizuri.

“KMC walitusumbua kipindi cha kwanza kwa kuwa wote walikuwa nyuma ya mpira walikuwa wanazuia tu lakini tulivyorudi cha pili tulitafuta njia za kuwafungua na kufanikiwa kupata mabao yote matatu,” alisema Matola.

SOMA NA HII  KIFAA CHA AS VITA CHAUKUBALI 'MZIKI WA YANGA'....AMTAJA MAYELE ...AFUNGUKA ISHU ILIVYO...