Home Habari za michezo YANGA KWAMBINDE SANA DHIDI YA NAMUNGO, MUDATHIR AFANYA MIUJIZA

YANGA KWAMBINDE SANA DHIDI YA NAMUNGO, MUDATHIR AFANYA MIUJIZA

Habari za Yanga

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Timu ya Yanga wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namungo Katika Uwanja wa Azam Complex leo Septemba 20.

Mchezo huo wa mzunguko wa tatu wa Ligi Kuu Bara umewashudia Yanga wakirudi kukamata usukani kileleni mwa msimamo wa Ligi baada ya kushushwa na Mashujaa waliokuwa na alama 7.

Ushindi huo wa Yanga unawafanya kuwa na alama 9 baada ya kucheza michezo mitatu na kushinda yote.

Yanga walisubiri mpaka dakika za lala salama kupata bao pekee la ushindi lililowekwa wavuni na Kiungo Mudathir Yahya dakika ya 88 akimalizia pasi safi ya Yao Kouassi.

Katika mchezo wa jana Klabu ya Namungo ilionekana kuwamudu Yanga vizuri sana tangu kipindi cha kwanza wakizuia kwa nidhamu ya hali ya juu.

SOMA NA HII  CHAMA, MOLOKO KUIKOSA NGAO YA JAMII ISHU IKO HIVI