Home Habari za michezo KISA UJIO WA KOCHA MPYA….RONALDO ATOA MSIMAMO WAKE MAN UNITED…”MAMBO LAZIMA YABADILIKE”…

KISA UJIO WA KOCHA MPYA….RONALDO ATOA MSIMAMO WAKE MAN UNITED…”MAMBO LAZIMA YABADILIKE”…


STAA wa kikosi cha Manchester United, Cristiano Ronaldo amesema kuwa kocha wao mpya, Eric ten Hag anahitaji muda na kuona anaacha alama ndani ya kikosi hicho.

Ten Hag anatarajiwa kutua United msimu ujao baada ya kumaliza majukumu yake ndani ya Ajax ambayo imetwaa ubigwa wa Ligi Kuu ya Uholanzi msimu huu wa 2021/22.

Wengi kwa sasa wanatarajia kuwa ujio wa kocha huyo unaweza kubadili mambo ndani ya kikosi hicho kwani timu hiyo imekuwa kwenye mwendo wa kinyonga.

Kwa muda wote huo wa misimu mitano timu hiyo inamaliza bila kutwaa taji jambo ambalo linawapa presha mashabiki pamoja na viongozi.

“Najua amefanya kazi kubwa ndani ya Ajax na ni kocha mwenye uzoefu ila anahitaji kupewa muda.Mambo lazima yabadilike kwa jinsi ambavyo anataka yeye,” amesema.

Bado haijajulikana hatma ya Ronaldo kama anaweza kubaki ndani ya kikosi hicho ama akasepa.

SOMA NA HII  PAMOJA NA DIRISHA KUFUNGWA...STAA SINGIDA BIG STARS ATEMWA MWEZI MMOJA BAADA YA KUSAJILIWA...